The House of Favourite Newspapers

Nabi Ampa Chico Ushindi Dakika 90

0

KATIKA kuhakikisha anafanya vema michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameiomba Kamati ya Mashindano kumpatia mchezo mmoja wa kirafiki.

 

Hiyo ni katika kujiweka fiti kipindi hiki ambacho Yanga haina mechi ya kimashindano hadi Machi 16, mwaka huu watakapocheza dhidi ya KMC kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Lengo la mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Jumamosi ya wiki hii ni kuangalia fitinesi ya wachezaji wake waliokuwa majeruhi akiwemo Chico Ushindi, Khalid Aucho, Shaban Djuma na Saidi Ntibazonkiza.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema mchezo huo wa kirafiki pia atautumia kuwapa nafasi wachezaji ambao wamekosa nafasi ya kucheza katika michezo ligi na Kombe la Shirikisho la Azam.

 

“Mchezaji mmoja akitumika kwa muda mrefu anachoka, hivyo ili kuhakikisha wachezaji hao hawapati uchovu, nimepanga kutengeneza mzunguko wakicheza kwa kubadilishana ili wengine wapate muda wa kupumzika.

 

“Kama unavyofahamu ligi ni marathoni, hivyo ni lazima kuwepo na mzunguko wa wachezaji kubadilishana katika baadhi ya michezo wakati tukiwa tunaelekea kumaliza msimu ambao ni mgumu.

 

“Hivyo basi ili hao wengine ambao hawakutumika kwa mfululizo katika michezo iliyopita, nitatoa nafasi kwao ya kucheza kwa kuanzia mchezo huu wa kirafiki tutakaoucheza kabla ya kucheza mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya KMC,” alisema Nabi.

WILBERT MOLANDI NA
MUSA MATEJA

Leave A Reply