The House of Favourite Newspapers

Nabii Suguye Kuliombea Taifa Liwe na Amani

0
Mchungaji Kiongozi Nabii,  Nicholaus Suguye wa Kanisa la The World of Reconciliation Ministries Ukonga jijini Dar Es Salaam akiwa katika Studio ya Global TV Online.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kulia) akifanya mahojiano na Nabii Suguye
Mahojiano yakiendelea.
Mhariri wa Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kushoto) na Sifael Paul (kulia) wakiwa na Nabii Suguye.
Dereva wa Nabii Suguye akimfungulia mlango wakati wakiondoka katika ofisi za Global Publishers Bamaga, Mwenge.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la The World of Reconciliation Ministries (WRM) lililopo Ukonga jijini Dar, Nabii Nicholas Suguye amesema anatarajia kufanya mkutano mkubwa wa kuombea amani ya nchi Septemba 27 hadi Oktoba Mosi mwaka huu katika Viwanja vya Hali ya Hewa Banana Dar.

 

Akizungumza na Global Tv On line jana, Nabii Suguye alisema atafanya hivyo kutokana na umuhimu wa amani katika nchi yetu.

 

Akizungumzi historia yake ya utumishi wa Mungu, Nabii Suguye alisema mara baada ya kupata wito wa Mungu wa kuwahudumia watu bila kujali dini zao,  aliamua kufuata maelekezo yake na kuanzisha kanisa  la WRM ambalo sasa lina waumini zaidi ya 5,000.

 

“Kanisa linajaa waumini, wapo wanaoketi chini na wengine juu ghorofani na wote hawa wanakuja kutokana na uhakika wa kazi za Mungu tunazofanya,” alisema Nabii Suguye.

Akizungumzia madai ya kuwataka  kulipia gharama fulani watu wanaokuja kufuata baraka na maombi yake kutokana na shida zinazowakabili, kiongozi huyo alisema analazimika kufanya hivyo kwa sababu ya gharama mbalimbali zinazotumika.

“Kuna fomu, wino, kalamu na wengine wanahitaji malazi, tuna nyumba maaluma wanalala wanaotoka mikoani, sisi hatulazi watu kanisani, pia kuna wahudumu wanaonisaidia, hayo yote yanahitaji fedha ndiyo maana tunawaomba watu wanaohitaji maombi kulipa sadaka kiasi fulani. Hili la sadaka sio agizo langu ni la Mungu mwenyewe na makanisa mengi duniani yanafanya hivyo,” alisema.

 

Aliongeza kuwa ndiyo maana kuna makanisa yana hospitali na shule kwa sababu ya sadaka wanazotoa waumini wao, hata hivyo alisema yeye ana shule ambayo aliianzisha hata kabla ya kuwa mchungaji.

 

“Nina televisheni ya WRM ambayo kazi yake kubwa ni kutangaza neno la Mungu na hivi sasa nimekuwa nikipata mialiko hata kutoka  nje ya nchi. Kwa hapa nyumbani nitafanya mkutano mkubwa wa kumuombea Rais John Magufuli na nchi yetu ili amani idumu Septemba 27 hadi Oktoba Mosi mwaka huu katika viwanja vya Hali ya Hewa Banana Ukonga na watu wa dini zote ninawakaribisha,” alisema Nabii Suguye.

Na Elvan Stambuli

Baada ya Bongo Muvi kufa Yafufuka kupitia (BARAZANI)

Leave A Reply