Nandy Ampigia Saluti Zuchu

 

MCHUMBA wa mtu anayefanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amempigia na kumpa heshima msanii mwenzake wa kike, Zuhura Kopa ‘Zuchu’ ambaye hivi karibuni alisainiwa rasmi kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Mondi’.

 

Mara tu baada ya Zuchu kusaini dili hilo, Nandy alitumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza mwanadada huyo akieleza imani yake kwake kuwa, ataufikisha muziki huu wa Bongo Fleva mbali.

Alimwandikia; “Hongera sana @officialzuchu am proud of you!!!!! Another QUEEN 👑  in Tz!!! Tusogezeeee Bongo Flevaaa mbali zaidi, nakuamini 🔥🔥🚨!”

 

Kitendo hicho kilisababisha watu kumpongeza Nandy kuwa, ni mwanamke wa tofauti na wengine ambao wangeishia kumponda Zuchu kwa kuwa ni mwanamke mwenzao.

“That’s what we call love, wanawake wakipeana support hivi, inatia moyo,” alichangia mada mmoja wa mashabiki wa Nandy.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Nandy anasema kuwa, siku zote kama unaona mwenzako anafanya kazi nzuri, lazima uikubali na kumpigia makofi.

Amesema anazijua vizuri kazi za Zuchu kwa muda mrefu na anazipenda.

 

“Mimi kama mwanamuziki, inaweza kuwa ngumu kusifia kazi za mwezangu, lakini kwa Zuchu, kiukweli anajua sana.

“Cha msingi ajitahidi kufanya vizuri, atafika mbali sana maana mimi ni shabiki wake pia,” amesema Nandy ambaye hivi karibuni alichumbiwa na mwanamuziki mwenzake, William Lymo ‘Billnass’.

 

STORI: IMELDA MTEMA, DAR


Toa comment