The House of Favourite Newspapers

Nandy: Billnass Amechangia 50% ya Mafanikio Yangu

0

MREMBO anayekiwasha kunako tasnia ya muziki nchini Tanzania, Nany The African Princess ameweka wazi kwamba, mchumba wake, Billnass anahusika kwa asilimia 50 kwenye mafanikio yake.

Nandy aliyasema hayo usiku wa kuamkia jana Jumapili baada ya kuangusha shoo yenye ujazo wake katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

“Huwa ananifanyia vitu vya pekee kila siku, ananishauri kila siku, amechangia asilimia 50 ya mafanikio yangu unayoyaona,” amesema Nandy.

Nandy ndiye aliyefunga shoo hiyo iliyokwenda kwa jina la Tanzanite Women Sports Festival 2021.

Wasanii wengine wakali wa kike waliofanya kweli ni Angela wa Konde Gang, Linnah, Lulu Diva, Malkia Hadija Kopa, Shilole, Rosa Ree na wengine kibao.

STORI: DENIS MTIMA, DAR

Leave A Reply