The House of Favourite Newspapers

Nandy Kufanya Balaa la Viwanja vya Posta, Dar

0

FAUSTINA Charles Mfinanga; unaweza kumuita Nandera au Nandy ametangaza balaa la kufa mtu leo, Jumamosi, Septemba 4, 2021 katika Viwanja vya Posta jijini Dar ambapo kutakuwa na lile tamasha lake kubwa la Nandy Festival 2021.


Akizingumza na Gazeti la IJUMAA jana
kuhusu maandalizi ya tukio hilo, Nandy au The African Princess alisema kuwa, kila kitu kipo sawia kabisa kwa ajili ya burudani ambayo ameahidi itakuwa ya kihistoria.

“Naomba nisiseme sana, lakini kama nilivyosema, Dar ndiyo kilele kikuu na Dar ndipo tunapoishi asilimia kubwa ya wasanii kwa hiyo itakuwa balaa juu ya balaa.

 

Mashabiki wafurike kwa wingi kwa sababu itakuwa hatari, kwa sasa tupo Jumba la Nandy Festival, maandalizi yote yamekamilika, kinachosubiriwa ni muda tu watu wakale burudani kama yote,” alisema Nandy ambapo listi ya wasafii watakaopafomu ni ndefu.

Leave A Reply