The House of Favourite Newspapers

Nandy: Nenga Asante Kwa Kunichagua

0

NANDY The African Princess ni mwanadada wa Kitanzania aliyejaaliwa kipaji kikubwa cha muziki na uigizaji. Kwa miaka kadhaa Nandy amejitengenezea umalikia wa Bongo Fleva kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki kutokana na nyimbo zake tamu zinazogusa hisia za wasikilizaji wake bila kujali rika kwani zinasikilizwa hadi na watu wazima.

 

Inafahamika kwamba, Nandy ni mchumba wa rapa mkali nchini Tanzania, Billnass au Nenga ambaye wamekuwa wakipita kwenye vipindi vya kupanda na kushuka kwa penzi lao.

 

Hata hivyo, kwa siku za hivi karibuni penzi lao limenoga kiasi cha kupewa majina tofauti na mashabiki kutokana na kuipenda kapo yao. Wikiendi iliyopita Nandy alivunja ukimya baada ya kumshukuru Nenga na kusema kuwa, Jumapili iliyopita ilikuwa ni siku kubwa kwao huku wengi wakiamini labda walikuwa wanafunga ndoa.

 

Nandy amemuandikia Nenga; “Asante kwa kunichagua, kesho (Jumapili) ni siku yetu special 20/2/2022! Sitokuangusha Billnass…”
STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply