The House of Favourite Newspapers

Nape Nnauye aipongeza Global

0

NAPE (2) Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist akimkaribisha Katibu Mwenezi wa CCM na Mbunge Mteule wa Jimbo la Ntama, Nape Nnauye.
NAPE (4) …Akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Global Publishers.
NAPE (8)Mwandishi wa Global Publishers, Brighton Masalu akimuuliza swali Nape Nnauye.
NAPE (5)Nape na Erick wakisikiliza swali kwa makini kutoka kwa mmoja wa wanahabari wa Global (hayupo pichani).NAPE (6)Nape akijibu swali.
NAPE (7)Wanahabari wa Global wakimsimsikiliza Nape.

napeNape akiendelea kufafanua jambo.
NAPE (1)Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo akimkaribisha Nape Nnauye.

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye leo amefanya ziara makao makuu ya Kampuni la Uchapishaji wa Magazeti Global Publisher yaliyopo Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutoa shukurani zake pamoja na chama kutokana na sapoti ya kampuni hilo kwa CCM kuanzia kampeni hadi kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.

Akichonga kupitia Global TV Online, Nape alisema Global ilikuwa sehemu ya ushindi wa chama hicho kutokana na kazi yake kubwa iliyoifanya ya kuufahamisha umma juu ya sera na kila kilichokuwa kinaendelea kwenye kampeni kutoka kwenye chama chake.

“Nawashukuruni sana jamani kwa kazi mliyoifanya ya kusimamia kile mlichokiamini, nawaahidi matokeo yake ni mabadiliko ambayo yatawanufaisha Watanzania wote ikiwemo wapinzani wetu wakuu Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao changamoto zao zitakuwa chachu ya maendeleo nchini,” alisema Nape.

PICHA NA RICHARD BUKOS, STORI NA BONIFACE NGUMIJE/ GPL

Leave A Reply