The House of Favourite Newspapers

Nape Nnauye: Wanahabari Tukutane Protea Hotel Saa 8 Kamili

Nape Moses Nnauye.

MBUNGE wa Jimbo la Mtama lililopo Mkoa wa Lindi, Nape Moses Nnauye, amechapisha ujumbe kwenye mtandao wake wa Twitter kuwataka wanahabari kukutana naye saa nane kamili Protea Hotel karibu na St. Peter Osterbay Dar es Salaam.

Aidha Nape amechapisha ujumbe huo ikiwa ni ujumbe wa pili baada ya ujumbe wa kwanza ambao ulisistiza wananchi na wanahabri kwa ujumla kutulia baada ya kutangazwa kwa Dk Harrison Mwakyembe kuwa ndiye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Comments are closed.