The House of Favourite Newspapers

Natasha afanyiwa oparesheni

0

NatashaMSANII mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ hivi karibuni alifanyiwa  oparesheni ya kuondoa uvimbe tumboni na sasa  yu kitandani anauguza kidonda.

Natasha alifanyiwa upasuaji huo wiki iliyopita katika  Hospitali ya Kairuki, Dar ambapo alitolewa uvimbe uliokuwa ukimsababishia maumivu ya tumbo kwa muda mrefu.

“Namshukuru Mungu kwa kuwa nimefanyiwa upasuaji na kutoka salama sasa nauguza kidonda na tatizo lilonisumbua zaidi ni presha kupanda, tumbo lilikuwa likinisumbua lakini nikawa napuuzia nilipokuja hapa ndipo ikagundulika ni uvimbe,” alisema Natasha akiwa hospitalini hapo siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji.

Leave A Reply