The House of Favourite Newspapers

Nay: Mimi Siyo Punda, ni Muziki tu

MMOJA kati ya marapa wanaofanya vizuri katika Bongo Fleva kwa sasa, ni Emmanuel Elibariki ambaye mashabiki wanamtambua vizuri zaidi kama Nay wa Mitego au kama mwenyewe anavyopenda kujiita, True Boy.

Ni msanii anayepata lawama nyingi kutoka kwa mastaa wenzake kuhusu namna anavyoufanya muziki wake, kwani mara kadhaa huwakejeli au kutaja mambo ya kweli wanayofanya wengine, wawe ni wanamuziki au wasanii wa fani nyingine.

Risasi Vibes lilimtafuta na kufanya naye mahojiano kuhusu masuala mbalimbali na yafuatayo ni baadhi ya maswali na majibu aliyoyazungumzia.

Una bifu lolote na Madee? Maana kuna post yako uliandika Instagram ni kama ilimlenga yeye?

Sina bifu na Madee na wala katika ile post sikumtaja mtu jina. Kilichotokea ni kuwa Madee amejitaja mwenyewe kutokana na maoni ya mashabiki.

Kwa nini mashabiki waamini ni Madee na si mwingine?

Inawezekana baada ya wao kusoma (Nay aliandika hivi; “Leo nimesikia wimbo mbaya, mtag mwenye huo wimbo.” Madee alitoa wimbo wake mpya wiki mbili zilizopita, Hela) wakaona ni yeye, lakini mimi sikumtaja mtu. Amedandia treni inayopita kwenye lami, siyo njia yake, mwache adandie afike. Life style yangu ni tofauti kabisa.

Lakini umekuwa na kawaida ya kuwaimba wenzio vibaya, kwa nini?

Siwaimbi vibaya, ila naimba vitu vina-vyoishi. Watu wanakariri kwa sababu ni mastaa. Bahati mbaya nikiwataja wasanii ndiyo wana-sema nawaimba wao, ila naimba kuhusu mambo mengi na watu wengi kwenye jamii na ninachokiimba nina uhakika nacho.

Una uhakika nacho? hebu thibitisha.

Angalia kwa mfano niliimba kuhusu mimba ya Wema, iko wapi? Nilisema kuhusu Ommy Dimpoz, nyinyi wenyewe mmesikia hivi karibuni nini kimetokea, yaani mambo mengi tu, lile gari la Shetta lipo? Na hata Ray si mmeona? (Wote hao aliwaimba katika wimbo wake wa Shika Adabu Yako)

Lakini huoni kama unakaribisha uadui na wenzako?

Ninahitaji maadui ili niendelee kusonga, watu kama hawa wasipokuwepo unaweza kubweteka. Nataka wawepo watu ambao wanasubiri nianguke ili wafurahi, sasa mimi nataka wasubiri sana, Nay anazidi kusonga mbele.

Unamaanisha maadui wasanii, ambao ni washindani wako au?

Sina msanii wa kufanya naye competition, nimeshawaacha mbali sana, sina mpinzani kabisa, maana waliokuwepo akina Chid Benz ndiyo kapotea, Madee, Nikki Mbishi nimewaacha mbali sana.

Watu wanasema unasafirisha unga, maana una utajiri ambao haufanani na thamani ya muziki wako, unasemaje?

Hata mimi nasikia watu wanazungumza hivyo, ni vizuri wakiendelea kuzungumza kwa sababu mimi naishi maisha yangu, kwa hiyo shauri yao, kama wao wananihisi hivyo na wanapotumia muda mwingi kunijadili, mimi naendelea, vitu vyangu vyote chanzo chake ni muziki.

Vipi ushkaji wako na Diamond, ni kama umefifia hivi?

Bado ni washkaji na tunawasiliana, tunapiga stori na tunapanga mambo, ila siku hizi tumebadilika, tukipiga picha hatuweki insta, tuko vizuri na muda ukifika kazi mpya itakuja.

Unaweza kufanya kazi na Ali Kiba?

Yaa, Kiba ni mshkaji mzuri, napiga naye stori kama kawaida na ishu yao na Diamond mimi hainihusu. Ikitokea kufanya naye kazi tunaingia mzigoni bila matatizo.

Kabla ya muziki ulikuwa unafanya nini?

Nilikuwa nacheza soka, mimi ni mchezaji mzuri wa mpira, lakini pia niliwahi kucheza Kick Boxing, kila nikipata nafasi napenda kuangalia huu

 

Comments are closed.