The House of Favourite Newspapers

NBC Yazindua Klabu ya Biashara Mtwara,Yatoa Mafunzo ya Biashara

0
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) Mtwara, Mh.Saidi Swallah (Kulia) akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa NBC Business Club mkoa
wa Mtwara.
Mmoja kati ya waliohudhuria kutoka TCCIA, Juma Napinda akitoa mada wakati wa tukio la uzinduzi wa NBC Business Club mkoa wa mtwara.

 

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea na mkakati wao wa kuzindua NBC Biashara Club katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania,ambapo hadi sasa wamezindua  klabu iyo katika maeneo kumi na mbili, na leo imezindua NBC Biashara Club katika mkoa wa Mtwara. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa NAF Beach Hotel, mkoani Mtwara na  mgheni Rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa TCCIA, Bw. Said Swallah.

 

Klabu ya Biashara ya NBC hutumiwa kama sehemu ya utunzaji wa biashara na mkakati wa uaminifu wa wateja. Kusudi kuu ni utoaji wa huduma za msaada zisizo za kifedha kupitia mafunzo ya ustadi wa biashara na kuwajengea uwezo kwa wateja wa biashara wa NBC, kama sehemu ya safari yetu katika kuwaunga mkono.

 

Akiongea katika hafla iyo, Kaimu Afisa Biashara office ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Bw. Amani Lusaki. aliipongeza NBC kwa kuja na wazo zuri la Biashara Club ambapo imewakusanya wafanyabiashara mbali mbali na kuwahamasisha, kuwaelimisha na

kuwafahamisha kuhusu fursa mbali mbali za biashara. Aidha alitaja kilimo cha Korosho, Mihogo na Ufuta kua ni moja wapo ya fursa za mkoa huo na kwa upande wa mifugo kunayo fursa kubwa ya nyama na maziwa. Aliitaka NBC Biashara Club kuwaunga mkono wafanya biashara wa Mkoa wa Mtwara kuzichangamkia fursa izi ili waweza kuinua uchumi wa mkoa huo.

 

Muheshimiwa mgheni rasmi, Bw. Said Swallah akizindua Club ya Biashara ya NBC, alisema walizungumzia fursa mbali mbali ikiwepo  kuuza bidhaa nje ya nchi, na jinsi ya kutumia biashara za mpakani zinazojulikana kama Cross Border Trade. Aidha taarifa kutowafikia watu imekua ni kikwazo, na kupitia forum ya namna hii  ameona dhahiiri wengi wanaweza kutumia nafasi hiyo kuingia na kufanya biashara izo na hatimaye kuingiza kipato na kukuza uchumi wa mkoa wa Mtwara.

 

“Tulianza biashara na watu wa Komoro katika kipindi kifupi sana na TCCIA wamekua  wakiratibu mawasaliano ya kibiashara kati ya Komoro na Mtwara, lakini wapo ambao walianza kufanya biashara baada ya nmeli kufika. Baadae meli zilianza kupungua baada ya muamko kupungua katika fursa iyo. Ni matumaini yangu kwamba kwa kupitia NBC Biashara Club, fursa kama izi hazitatupita tena.” Alisema Bw. Said Swallah.

 

Naye  Meneja wa bidhaa na huduma za kifedha NBC Makao makuu Dar es salaam, Bw. Jonathan

Wilson Bitababaje alimalizia uzinduzo huo kwa kusema, wamezingua club iyo kwa lengo kubwa la kuwaleta wateja wao pamoja ili waweze kuungana katika eneo la biashara na pia kuwapa mafunzo wateja wao wa NBC ili wapate elimu kubwa sana ya kuzikuza biashara zao, na waweze kuendesha biashara zao katika hali ya ushindani na soko la nje ya nchi. “Tunawapa mafunzo ya ndan ni pia tunawapa mfiduo ya kwapeleka nje nchi kukutana na wafanya biashara wakubwa na wenye viwanda vikubwa iliwaweze kua wanaagiza bidhaa na kupata moja kwa moja kutoka viwandani.”

 

Mwisho alisema, “Tulikua na semina nzuri leo na tumewafundisha namna ya kuendesha biashara kifaida na kukuza mitaji yao, na bidhaa ambazo tunazo benki zinazoweza kuwasaidia wao kupata biashara apa eneo la Mtwara. Lakini pia tumepata fursa nyingi sana ambazo wafanya biashara wetu wanaweza kuzipata katika eneo zima la Mtwara na sisi kama benki tuko tayari kabisa kuwasaidia.”

 

Wateja wa NBC wanayo fulsa ya kupata huduma na bidhaa bora mbalimbali za kibenki zenye uwezo wa kukidhi mahitaji yao yote muhimu ya kibiashara na kifedha kama, Mikopo ya aina mbalilmbali, Bank Guarantee za aina mbalimbali, Huduma za bima mbalimbali, Kununua na kuuza fedha za kigeni, Internet Banking na Kutoa ushauri na mafunzo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali.

Leave A Reply