The House of Favourite Newspapers

Ndege Mpya Airbus A220-300 Kutua Bongo Jumapili

Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema Serikali itapokea ndege yake nyingine mpya toleo la Airbus A220-300, Jumapili hii Desemba 23, 2018.

Abbas ameeleza hayo leo Ijumaa, Desemba 21, 2018 katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

“Ungana nasi kuipokea ndege ya kwanza kununuliwa na Serikali kwa toleo la Airbus A220-300. Ni Tanzania pekee.’Ngorongoro-Hapa kazi Tu’, itawasili nchini Jumapili hii na siku chache baadaye ndege nyingine kama hiyo itawasili Dodoma-Hapa Kazi Tu,” ameandika Dk Abbas.

Ndege hizo mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) zimetengenezwa nchini Canada na zimeshafanyiwa majaribio hivyo zikitua nchini zitapangiwa route ya safari zake.

Comments are closed.