The House of Favourite Newspapers

Ndege Yaanguka Barabarani

0

ZAIDI ya watu 100 wamenusurika kufa baada ya ndege ya abiria kuanguka katikati ya barabara katika mji wa Mahshahr nchini Iran asubuhi leo.

Ndege hiyo aina ya Caspian 6936 ilikuwa na  watu 135 ikitoka Tehran na ilitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mahshahr.

Ndege kama hiyo ilianguka mwaka 2009 katika mji wa Qazvin kaskazini magharibi mwa Iran na kusababisha vifo vya abiria 153 na wahudumu 15.

Leave A Reply