The House of Favourite Newspapers

Ndege Yapotea na Rubani Ruvuma

0

NDEGE ya Shirika la Uhifadhi Pams Foundation Aina ya Bathawk 5HWXO iliyokuwa ikisaidia kutafuta Faru Weusi katika Pori la Akiba la Selous Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imepotea kwa siku 11 ikiwa na Rubani wake Bw. Samweli Gibuyi.

 

Mkuu wa Wilaya Tunduru Bw.Julius Mtatiro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado wanaendelea na juhudi za kumtafuta rubani huyo.

 

“Napenda kuthibitisha kuwa hadi saa ndege hiyo iliyokua inaruka kutoka anga la matemanga Tunduru ikielekea Kingupira kwa kupitia hifadhi ya Selous lakini pia kutipia anga la Liwale, ndege hii haikutua na mpaka leo siku ya 10 hatujampata ndugu yetu na pia haujapata chombo hicho” DC Mtatiro.

 

Ameongeza kusema kuwa chombo maalum ambacho kinatumika kurekodi kumbukumbu za ndege kinachojulikana kwa jina la SpiderTracks, hakijarekodi mwenendo wa chombo hicho.

 

Aidha ametoa rai kwa wananchi wote wa Kusini kutoa ushirikiano pindi watakapo pata taarifa zozote zinazoashiria uwepo wa chombo hicho ama Rubani huyo.

Leave A Reply