The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Coletha Yapigwa Kalenda

Coletha Raymond

NDOA ya muigizaji nyota Coletha Raymond iliyokuwa ifungwe mwishoni mwa mwezi huu, sasa imepigwa kalenda hadi AprilI kwa sababu zisizoepukika. Coletha aliliambia Risasi Mchanganyiko kuwa sababu kubwa ya kusogezwa mbele kwa ndoa hiyo ni uwepo wa Kwaresma, kitu ambacho kwa mujibu wa dini ya Kikristo, jambo hilo halipaswi kufanywa wakati huo.

  “Tulikuwa tumeshafanya maandalizi yote vizuri na kwa kweli tulikuwa tunasubiri siku tu, lakini bahati mbaya tulisahau kuwa mwezi huu ni Kwaresma, ndiyo maana tukaona tusogeze hadi AprilI na kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa,” alisema muigizaji huyo anayetarajiwa kufunga ndoa na mtu anayefahamika kwa jina moja la Temba.

Comments are closed.