The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Davido, Chioma Yanukia, Waenda Ukweni Owerri

MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria, Davido, na mchumba wake Chioma, wanaelekea katika  kukamilisha uvumi wa penzi lao — kufunga ndoa hivi karibuni.

Katika kulionyesha wazi penzi leo, wawili hao walifuatana hivi karibuni  — katika ndege binafsi ya bwanaharusi huyo mtarajiwa — alipokwenda kutumbuiza huko Cotonou, Benin.

Kituo kilichofuata ni Oweri, Jimbo la Imo, ambalo ndilo nyumbani kwa bibi harusi huyo mtarajiwa na msomi wa chuo kikuu.

Huu ndiyo mwanzo wa kumalizika kwa mashaka ya utabiri wa kuoana wawili hao, kwani kengele za ndoa zimeanza kusikika “kwa mbali”.

Comments are closed.