The House of Favourite Newspapers

NDOA YA DAVIDO YANUKIA

WAKATI tetesi zikizidi kutapakaa kuwa mrembo Chioma ni mjamzito, Davido ameanza mipango ya kufanikisha ndoa yake na mrembo huyo ambayo huenda ikafanyika mwakani 2020.

 

Kupitia kwenye mtandao wake wa Instagram, Davido ame-share picha iliyoambatana na ujumbe uliosomeka” First of all introduction” ikiwa ni ishara kwamba utambulisho ulishafanyika na sasa inasubiriwa ndoa tu.

 

Kaka mkubwa wa Davido ambaye naye ametangaza kufunga ndoa mwakani, Adewale Adeleka, ametuma ujumbe kwenye Instagram yake kuipongeza ‘couple’ hiyo ambayo imeanza kuwa maarufu sana mtandaoni.

Comments are closed.