The House of Favourite Newspapers

Ndonga za Global TV Sasa Kupigwa Jumapili

0

KUFUTIA maombi ya wadau mbalimbali nchini, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), chini ya rais wake, Yassin Abdallah ‘Ustaadh’, imeamua kusogeza mbele mapambano ya Kimataifa ya Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati.

Mapambano hayo sasa yatapigwa Julai 23, mwaka huu badala ya Julai 22, huku yakirushwa mubashara na kituo cha Global TV Online.

Mapambo hayo yameandaliwa na kampuni ya kupromoti ngumi nchini, Solid Rock Promotion, na yatafanyika kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar na kurushwa mubashara na Kituo cha Global TV Online kupitia webiste yake ya www. globaltvtz.com

Rais Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustaadh’,

Bondia wa Tanzania, Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ atapambana na Israel Kamwamba, Idd Pialali dhidi ya Regin Champion raia wa DR Congo, wakati Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ akitarajia kucheza na Tinashe Mwadziwana kutoka nchini Zimbabwe. Mapambano hayo yote ni ya raundi kumi.

Rais wa TPBO, Ustaadh alisema kuwa wameamua kusogeza mbele mapambano hayo kufuatia kupokea maombi ya wadau waliotaka yapigwe siku hiyo.

“TPBO ilipanga mapambano yafanyike Julai 22, mwaka huu lakini tumeamua kufanya mabadiliko kidogo ambapo sasa yatafanyika Julai 23 kama walivyoomba wadau. Suala la kurusha mubashara litabaki kama lilivyo kwa upande wa Global TV,” alisema Ustaadh.

Stori: Ibrahim Mussa | Championi

Leave A Reply