The House of Favourite Newspapers

Spika Afanya Mabadiliko ya Wajumbe Kamati za Bunge

0

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amefanya mabadiliko  madogo ya wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 imeeleza kuwa mabadiliko yamefanyika kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 135 (3) – (5) ya kanuni za kudumu za Bunge toleo la Juni 2020.

 

Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amehamishiwa kutoka kamati ya utawala na Serikali za mitaa kwenda kamati ya sheria ndogo.

 

Mabadiliko mengine ambayo Spika ameyafanya ni kumhamisha Godwin Kunambi kutoka kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama kwenda kamati ya ardhi, maliasili na utalii.

 

Pamoja na hao Spika amewateua baadhi ya wabunge katika kamati kadhaa ambapo Asia Halamga na Agnes Marwa wamepelekwa kamati ya masuala ya Ukimwi.

 

Pia, amemteua Dkt. Faustine Ndugulile kuwa mjumbe wa kamati ya sheria ndogo na kamati ya masuala ya Ukimwi Dkt. Medard Kalemani na Dk Leonard Chamuriho wameteuliwa kuwa wajumbe wa kamati ya sheria ndogo.


Leave A Reply