The House of Favourite Newspapers

Ndugai Atoa Salamu za Rambirambi Kifo cha Mapacha Maria, Consolata

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ametuma salamu za pole kwa familia ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti, waliofariki dunia juzi Jumamosi (Juni 2, 2018) usiku, katika Hospitali ya Mkoa ya Iringa walikokuwa wakitibiwa.
Ndugai ametoa salamu hizo leo bungeni jijini Dodoma, muda mfupi baada kumalizika kipindi cha maswali na majibu. na kusema;
“Natoa salamu za rambirambi kwa familia ya watoto hawa Maria na Consolata na mazishi yao inaweza kuwa leo huko Iringa. Walikuwa watoto wenye upendo sana. Kifo chao ni wazi kimetuumiza sote. Waziri wa Elimu (Profesa Joyce Ndalichako) tufikishie pole zetu huko,” alisema Ndugai.

Comments are closed.