The House of Favourite Newspapers

Ndugai Awaomba Radhi Wakristo Kwa Kauli Yake

0

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewaomba radhi Wakristo kwa kauli aliyotoa leo Bungeni alipokuwa akielezea alivyotembelea Israel

Katika maelezo yake alisema “Yesu alitembea na mke wake kutoka Nazareti kwenda Yerusalemu kuhesabiwa” ambapo amesema alimaanisha Yusufu alitembea na mke wake, sio Yesu kama alivyotamka

Amesema kilichotokea ni kosa la kibinadamu wakati alipokuwa akieleza kuwa anaufahamu ukristo vizuri na kuwa amewahi kuhiji maeneo matakatifu

Leave A Reply