The House of Favourite Newspapers

Ndugai: Bunge Lipo Tayari Kurekebisha Tozo

0

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge liko tayari kufanya marekebisho yatakayohitajika kwenye tozo za miamala ya simu zilizopitishwa wakati wa Mkutano wa Bunge.

Amesema, “Labda katika nia njema ile kuna maeneo hatukuangalia vizuri, basi tutajaribu kutazama vizuri huko tunapokwenda kama Rais Samia alivyoelekeza. Tukiondoa tozo tumeacha gizani malengo yetu yote tuliyotaka kufanya….”

Ameeleza kuwa dhamira ya Bunge kupitisha tozo hizo ilikuwa kupata fedha zitakazoelekezwa kusaidia Ujenzi wa Madarasa ya Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.

 

Leave A Reply