The House of Favourite Newspapers

NEYMAR ALIPANIA KOMBE LA DUNIA 2022

0

STAA wa Brazil na Klabu ya Paris Saint Germain, Neymar Jr amefunguka kuwa sasa ndoto yake ni kucheza Kombe la Dunia na kufanya kweli mwaka huu.

 

Kombe la Dunia linatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu nchini Qatar na Brazil imefanikiwa kufuzu kushiriki michuano hiyo.

 

Brazil imepangwa katika Kundi G ikiwa na timu za Cameroon, Serbia na Uswisi na michuano hii itafanyika mwishoni mwa mwaka huu.

 

Hii itakuwa sio mara ya kwanza kwa Neymar kushiriki, kwani tayari amecheza Kombe la Dunia mwaka 2014 na 2018 japo huenda ikawa michuano yake ya mwisho kama yeye mwenyewe alivyowahi kunukuliwa hapo nyuma.

 

Neymar alisema: “Ndoto yangu kubwa kwa mwaka huu ni kuona nafanya kitu katika Kombe la Dunia. Ukweli nilikuwa nataka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini ndoto hiyo ilipotea kwani tulishindwa kutamba ndani ya UEFA.

 

“Ninaamini na matumaini yangu ni mwaka 2022 kwangu unaenda vizuri kwenye Kombe la Dunia.”

Leave A Reply