The House of Favourite Newspapers

Ni Wikiendi ya Mtikisiko Dar Live

0

IJUMAA | SHOWBIZ

WIKIENDI hii pale kwenye Uwanja wa Taifa wa burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar patakuwa hapatoshi kufuatia kuwepo kwa shoo zilizoongozana.

Hii ina maana kwamba, kesho (Jumamosi) Bendi ya Jahazi Modern Taarab ikiongozwa na mastaa wake, Leila Rashid, Amigo, Mwasiti Kitolonto, Ally J, Fatuma Kassim na wengine kibao watadondosha bonge la shoo kisha Jumapili kutakuwa na concert iliyopewa jina la Wali Mende.

KUHUSU KESHO (JUMAMOSI)

Kiongozi wa Bendi ya Jahazi, Amigo alisema kuwa watafanya shoo ambayo hawakuwahi kuifanya sehemu yoyote hivyo watu wajitokeze kwa wingi.

“Tutalisimamisha Jiji la Dar kwa muda kwa kufanya mambo tofauti kabisa, mashabiki wetu wote waje kwa wingi,” alisema Amigo.

Kuhusu mtonyo, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kiingilio ni shilingi 6,000 tu, yaani kama bure vile.

Ditto.

JUMAPILI SASA

Kutakuwa na shoo iliyoandaliwa na Kituo cha Redio cha EFM kupitia Kipindi cha Ladha 3600. Mratibu wa mpango mzima, Jabir Saleh a.k.a Kibonge Tozi alisema siku hiyo ya shoo Kipindi cha Ladha 3600 kinatimiza mwaka mmoja, hivyo kwa kushirikiana na Dar Live wamepanga kutoa burudani ya nguvu.

“Tunajivunia kutimiza mwaka mmoja, tunarudisha fadhila kwa wasikilizaji wetu, wasanii watakaokamua ni Dogo Ditto, Pam D, Chin Beez, Tammy the Baddest na Hussein Machozi atakayefanya shoo yake ya kwanza nchini akitokea Italia,” alisema Kibonge Tozi.

Leave A Reply