The House of Favourite Newspapers

Nick Cannon agomea talaka ya Mariah carey

0

nickcannonNick Cannon.

Mume wa Mwanamuziki Mariah Carey, Nick Cannon juzikati aligoma kusaini karatasi za kuidhinisha kumpa talaka mkewe huyo kwa madai kuwa hayuko tayari.

Kinachoonekana Nick bado anampenda mama watoto wake huyo hivyo hayuko tayari kumuona akiolewa na tajiri James Packer ambaye amemvalisha pete ya uchumba kwa lengo la kufunga naye ndoa.

attends the 2008 Whitney Museum of American Art's gala and studio party at the Whitney Museum of American Art on October 20, 2008 in New York City.Nick Cannon na Mariah Carey.

Nick na Mariah walitangaza kutengana Agosti, 2014 na miezi michache baadaye walifungua mafaili ya talaka mahakamani lakini Nick anataka kumfanyia mbaya Mariah kwa kutotaka kumpatia talaka ili kukwamisha zoezi la ndoa.

“Nick bado ana mapenzi na Mariah na hayuko tayari kumpoteza, hata alipovalishwa pete ya uchumba aliumia mpaka akafikia hatua ya kulazwa hospitali, hiyo ni pete tu, ndoa je?” alisema rafiki wa karibu wa mastaa hao alipokuwa akizungumza na mtandao mmoja wa habari za mastaa.

Mariah na Nick walifunga ndoa ya siri mwaka 2008 kwenye Visiwa vya Nahamas na wana watoto wawili mapacha, Moroccan na Monroe.

Leave A Reply