The House of Favourite Newspapers

Mpaka Home: Nicole Apata Kigugumizi Kumzungumzia MC Pilipili

0

NA MAYASA MARIWATA | RISASI JUMAMOSI| MPAKA HOME

KAMA ilivyo kawaida ya kolamu hii ya Mpaka Home kuwatembelea mastaa mbalimbali na kuangalia wanavyoishi majumbani mwao, leo tumefika kwa msanii wa filamu za Kibongo, Nicole Franklyn anayeishi Kinyerezi, Dar.

Nicole ambaye pia ni Miss Shinyanga mwaka 2014 pia aliyeingia Top 5 ya Miss Tanzania mwaka huohuo ameeleza mambo mengi anayopenda kuyafanya anapokuwa nyumbani kwake hapo.

MPAKA HOME: Naona nyumbani kwako pako kimya sana, unaishi peke yako?

NICOLE: Hapana, ninasishi na mtoto wangu na dada wa kazi.

MPAKA HOME: Ratiba zako za siku zikoje?

NICOLE: Kwanza kabisa nikiamka tu asubuhi nafanya usafi wa nyumba yangu baada ya hapo napata kifungua kinywa  kisha naenda kwenye shughuli zangu.

MPAKA HOME: Ukiwa nyumbani unapenda kufanya nini?

NICOLE: Napenda kupika na kutazama muvi.

MPAKA HOME: Ni muvi gani ambazo umewahi kufanya tangu ujikite kwenye sanaa?

NICOLE: Nimecheza Filamu ya Red Flag na Get Keeper.

MPAKA HOME: Umesha wahi kuwa kwenye uhusiano na msanii?

NICOLE: Sijawahi na sifikirii.

MPAKA HOME: Mbona kuna madai kuwa ulishawahi kutoka kimapenzi na MC Pilipili, hilo likoje? NICOLE: Sitaki kuzungumzia mambo ya nyuma, niulize kuhusu mambo yangu ya sasa.

MPAKA HOME: Wewe ni miongoni mwa wasanii waliokumbwa namaumivu ya mapenzi baada ya baba mtoto wako ambaye ni mbunge kukusaliti, je ulishawahi kutamani kujiua kwa sababu hiyo?

NICOLE: Naanzaje kufanya ujinga huo? Siwezi kuthubutu maana dunia ina raha yake.

MPAKA HOME: Mbali na sanaa unajishughulisha na nini?

NICOLE: Ninafanya biashara lakini pia ni mtangazaji wa TV E ya EFM.

MPAKA HOME: Maisha yako yapoje baada ya kujifungua na kutelekezewa mtoto?

NICOLE: Ni ya furaha mno, si unajua mtoto ni zawadi tosha kutoka kwa Mungu hivyo naona kawaida tu.

MPAKA HOME: Unapenda kuwa na mwanaume wa aina gani ambaye unaamini atakufuta machozi?

NICOLE: Sina machozi maana maumivu kwenye mapenzi ni kawaida ila napenda mwanaume mcha Mungu, mchapakazi na mwenye mapenzi ya kweli kwangu.

Leave A Reply