The House of Favourite Newspapers

JPM AMPA LUGOLA MTIHANI WA LUGUMI – VIDEO

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri Mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kusimamia vilivyo wizara hiyo ikiwemo kufuatilia na kubaini mapungufu kwenye mikataba iliyoingiwa na Jeshi la Polisi nchini likianzisha miradi mbalimbali na kuchukua hatua stahiki.

 

Magufuli ameyasema hayo leo Julai 02, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuwaapisha viongozi aliyowateua jana Jumapili kuziba nafasi za viongozi wengine aliyowaengua na waliostaafu.

 

“Wizara ya Mambo ya Ndani kuna mambo ya hovyo yanafanyika, viongozi wa juu wa wizara hiyo sijaona wanachokifanya, sijawa impressed na hii wizara. Kuna mradi wa Lugumi ulianzishwa na Jeshi la Polisi, vipo baadhi ya vituo vya polisi havijakamilishiwa mradi huo, serikali tulipewa maelekezo nini cha kufanya, lakini mpaka sasa niliyowateua sijaona chochote kilichofanyika, nakuagiza waziri (Lugola) ukalifuatilie hili na hatua zichukuliwe haraka.

 

“Kuna suala la NIDA, huko pesa zilichezewa, tukachukua hatua, wapo watu walifanya mambo ya hovyo tukawasimamisha kazi, vifaa vingine viliagizwa na havikufika, waliofanya hayo hawajashughulikiwa, TAKUKURU naona wanapachezeachezea, tuliowasimamisha hawajashughulikiwa.

 

“Wafungwa wakafanye kazi, huwezi kumfunga mtuhumiwa jela halafu ukamlisha, walime, hata waliohukumiwa kunyongwa, kwa nini waziri ameshindwa kupeleka hata muswada bungeni kubadili hiyo sheria ili na wao wafanye kazi? Hadi Bunge limeisha.

 

“IGP Simon Sirro palikuwa na majambazi sasa yamepungua, wakati mwingine unamuona anakimbia mchakamchaka huko, ndiyo kazi zenyewe za kuwatumia wananchi. ,” alisema Magufuli.

Na Edwin Lindege | Global Publishers.

VIDEO: FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA

 

Comments are closed.