The House of Favourite Newspapers

Nisha awahofia wakware kwa mwanaye

0

nishaa.jpgStori: Gladness Mallya

MSANII anayefanya vizuri katika filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefungukia hofu aliyonayo kwa mwanaye, Ipsium kutokana na wanaume wakware kuzidi kuongezeka kila siku.

Akichonga na Risasi Vibes, Nisha alisema hata akiwa na ‘boyfriend’ wake, huwa hapendi amzoee mwanaye huyo, kwani anamlea katika maadili ya kidini zaidi na anamshukuru Mungu anazingatia vile anavyotaka.

“Mwanangu yuko darasa la saba na analala shuleni lakini wakifunga, huwa anarudi nyumbani hivyo kwa kuwa nasafiri mara nyingi, huwa nawapeleka yeye na dada wa kazi kwa mama yangu ili kuepusha wanaume wakware wasiniharibie mwanangu maana nina hofu sana na wanaume wakware,” alisema Nisha.

Leave A Reply