The House of Favourite Newspapers

Nisha Azindua Nyumba Yake Mpya – Video

0

Usiku wa kuamkia leo mwigizaji maarufu wa vichekesho nchini, Salma Jabu maarufu kama Nisha amezindua nyumba yake aliyoijenga maeneo ya Goba Dar es salaam iliyogharimu zaidi ya Tsh. milioni 100 ambayo anasema ndio imekua ni nyumba ya ndoto zake.

 

Nisha anasema; “Ilikuwa ndoto yangu, nilijinyima nikapoteza mpaka mashabiki lengo ilikuwa nikutimiza hili, nimeanza kujenga tangu mwaka 2018 niliponunua kiwanja, unajua Wasanii tunaishi maisha ya kufeki nilichoka kupanga, ramani nimechukua kwenye moja ya mjengo niliowahi kupanga.”

 

“Wenye nyumba walionipangishaga wamekuja na wamefurahi kuniona na kwangu sasa, nimejenga kwa hela za movie lakini pia Nishass Wedding vilevile michezo ya kuweka hela na kukopa ya kina Mama imesaidia, kwa wengine hii inaweza kuwa ndogo lakini kwangu ni kubwa sana na nina mshukuru Mungu sana.”

 

Leave A Reply