The House of Favourite Newspapers

Niva: Wema ni Tajiri, Hataki Kujionesha

0

MREMBO ambaye ni nembo ya tasnia ya Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu; historia yake ni ya kuigwa na ni tofauti mno.

Kumbuka mrembo huyu ndiye aliyechangia pakubwa mno kujulikana kwa supastaa wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz.

 

Kwa mujibu wa mwigizaji mwenzake wa kiume, Niva Super Marioo, Wema ni mwanamke tajiri mno.

“Ana nyumba za kifahari na magari aina tofauti. Anapata pesa zake kupitia filamu na pia ubalozi katika bidhaa tofauti.

 

“Wema ni tajiri, lakini hapendi kujionesha, ameshapita kwenye steji hiyo ya kujionesha,” anasema Niva.

Kauli ya Niva inakuja wiki moja baada ya kuibuka kwa mjadala mkali mno juu ya kauli iliyotolewa na Aristote; chawa wa mwigizaji Irene Uwoya kwamba mrembo huyo amefulia kiasi cha kushindwa hata kumiliki gari.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply