The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Kocha Kanichezesha Nikiwa Mgonjwa

0
Kiungo mchezeshaji wa Simba, Haruna Niy­onzima Jumapili.

Kiungo mchezeshaji wa Simba, Haruna Niy­onzima Jumapili iliyopita alitumiwa na kocha wa timu hiyo, Joseph Omog kwenye pambano dhidi ya Mbeya City akiwa anaumwa.

 

Simba Jumapili iliyopita iliende­lea kujikita vyema kileleni mwa Ligi Kuu Bara, baada ya kuibamiza Mbeya City bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine na kuifanya kufikisha pointi 19 sawa na Azam FC, wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Niyonzima alisema, kwamba kisa cha kutocheza dakika 90 za pambano hilo ilitokana na kocha huyo kumpumzisha kwani alimchezesha akiwa na homa kali.

 

“Ujue kisa cha kutocheza dakika zote katika mchezo wetu na Mbeya City nilicheza nikiumwa baada ya kocha kunihitaji sana nicheze nikiwa katika hali hiyo kufuatia ukubwa wa mchezo wenyewe.

 

“Nilicheza kwa taabu sana ingawa ilikuwa ngumu sana kwa mashabiki kugundua kwani nilikuwa naumwa na kichwa sana siku hiyo na pia niliingia nikiwa na mawazo ya msiba wa mama yangu wa kambo ambaye ni mlezi wangu mkubwa,” alisema Niyonzima.

Stori: Musa Mateja

Leave A Reply