The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Mavugo Hakosi Timu

0
Mavugo akimbeba Kichuya.

WAKATI tetesi za kutemwa kwa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo, kiungo mchezeshaji wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kukosa timu kama akiachwa.

Mavugo ni kati ya wachezaji wali­opo kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo la msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kwa kile ki­nachotajwa kiwango chake kushuka.

Mrundi huyo, tayari ameanza kunyatiwa na baadhi ya klabu za nje ya nchi na kati ya hizo ni Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Niyonzima alisema Mavugo bado ana uwezo mkubwa wa ku­funga mabao, lakini vitu vidogo ndiyo vinamfanya ashindwe kutimiza maju­kumu yake.

Niyonzima alisema, mshambuliaji huyo ki­nachomfanya ashindwe kucheza ni presha kubwa iliyopo kwenye timu huku akimtabiria kuwa akienda kwingine atacheza vizuri.

“Mavugo siyo mbaya kiasi hicho, binafsi naona ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufun­ga mabao katika timu.

“Lakini kitu kikubwa ki­nachomfanya ashindwe kucheza vizuri ni presha iliyopo katika timu pekee na siyo kitu kingine.

“Ninakuhakikishia akien­da timu nyingine tofauti na Simba atakuwa tege­meo, kwani ana uwezo mkubwa,” alisema Niyonz­ima.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam | Championi.

VIDEO: MSHUHUDIE MASAU BWIRE AGEUKA MFALME

Leave A Reply