The House of Favourite Newspapers

Niyonzima, Morrison Wampasua Kichwa Kocha Namungo

0

KOCHA wa Namungo, Thierry Hitimana amesema kikosi chake kimejipanga vilivyo kuwaliza Yanga lakini alivyokumbuka tu ndani ya kikosi hicho kuna wachezaji kama Benard Morrison na Haruna Niyonzima ghafla akaingiwa na hofu.

 

Namungo inatarajia kucheza na Yanga kesho Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi ambapo timu hiyo inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 49 huku Yanga ikiwa kwenye nafasi tatu na pointi 50.

 

Niyonzima na Morrison ni kati ya wachezaji walioonyesha uwezo mkubwa kwenye Dabi ya Kariakoo iliyoisha kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Morrison.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Hitimana alisema kuwa, wamejipanga kupata ushindi katika mchezo kutokana na maandalizi yao lakini bado wanapresha kubwa ya wapinzani wao kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa katika mechi yao na Simba.

 

“Binafsi naamini hautokuwa mchezo rahisi siyo kama tulivyokutana msimu uliopita katika kombe la FA na wakati ule bado tulikuwa tunacheza daraja la kwanza, malengo yetu ni kuona tunafanikiwa kushinda mchezo kutokana na maandalizi yetu yalipofikia sasa.

 

“Lakini suala la presha lipo juu naamini hata wao wanajua wanakuja kucheza na timu bora, lazima iwe hivyo na ukiangalia kiufundi katika mechi yao na Simba walikuwa bora zaidi, wachezaji wote walicheza kwenye kiwango kikubwa na hatujui kama watakuja kwetu kwa nguvu ile ila sisi tunataka kushinda,” alisema Hitimana.

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Leave A Reply