The House of Favourite Newspapers

Niyonzima Sasa Aanza Kuwaza Ubingwa

0

KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda amefunguka kuwa, iwapo watashirikiana kwa pamoja wachezaji wote na benchi la ufundi ana uhakika wa timu yake hiyo kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

 

Niyonzima amesajiliwa katika usajili wa dirisha dogo kwa lengo la kuongeza nguvu katika kikosi hicho kuhakikisha kinafanya vyema na kutwaa ubingwa wa ligi.

 

Yanga kwa sasa ipo nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi ikiwa na pointi 37, huku wakiwa  wamepishana pointi 16 na watani wao Simba wenye pointi 50.

 

Hii ni kabla ya mechi za jana. Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima alisema kuwa, kama mchezaji dhamira yake ni kuonyesha kile alichonacho ndani yake kwa kuisaidia timu ili iweze kufanya vizuri kwenye ligi kwa kushirikiana na wenzie

 

“Nafasi ya ubingwa kwa Yanga bado ipo licha ya kutanguliwa katika msimamo wa ligi, tukishirikiana kwa pamoja bado tuna nafasi sana ya kuweza kufika kule tunapopahitaji, tuna kikosi kizuri na chenye ushindani.

“Kwa upande wangu najitahidi kuonyesha kile ambacho naona ni kizuri kwa manufaa ya timu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,” alisema Niyonzima.

 

 

Leave A Reply