The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Sasa Msuva Atakuwa Mfungaji Bora

NIYONZIMA (7)

Mshambuliaji wa timu ya Yanga.

Wilbert Molandi | Championi Jumatano

NAHODHA na kiungo mchezeshaji wa Yanga Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amejiapiza kuwa, kwa mfumo huu aliokuja nao kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia, Goerge Lwandamina utamnufaisha winga, Simon Msuva kufunga mabao mengi.

 Hayo, aliyasema baada ya kutengeneza nafasi tatu za mabao matatu katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara walipovaana na JKT Ruvu na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mnyarwanda huyo, katika nafasi hizo alizozitengeza mbili zilikwenda kwa Msuva na kuzitumia vizuri kwa kufunga mabao mawili pekee yote akiyafunga kipindi cha pili. Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima alisema mfumo huo mpya wa Lwandamina umempunguzia yeye majukumu kutokana na kupewa jukumu kupiga pasi za mwisho za mabao huku jukumu la kukaba likiwa la Thabani Kamusoko na Said Makapu ambaye aliingia kipindi cha pili kwenye mechi na Ruvu. “Nikwambie kitu, Msuva
Kotei anajua kunisoma na mimi ninajua aina ipi ya pasi anazozihitaji nimpasie tukiwa tunacheza pamoja kutokana na kasi yake aliyonayo. 

“Hivyo, ninakuhakikishia kuwa Msuva atafunga sana kutokana na majukumu niliyopewa na Lwandamina na mfumo anaotaka niutumie wa kupiga pasi nyingi za mbele pale ninapokuwa nina mpira miguuni mwangu. 

“Kama unakumbuka mechi na Ruvu nilianza kwa kucheza namba 8, lakini kipindi cha pili kocha akanibadilisha na kucheza 10 na alifanya hivyo baada ya kuona pasi nyingi haziendi golini mwa wapinzani na alivyonibadilisha ukaona tukapata mabao mawili yote yakitoka mguuni mwangu yaliyofungwa na Msuva, naamini kwa mwendo huu atakuwa mfungaji bora,”alisema Niyonzima nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.