The House of Favourite Newspapers

NMB Bonge la Mpango Yaja Kivingine, Yamwaga Mil 246

0
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati), akizindua promesheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, ikiwa na lengo la kuhamashisha nidhamu ya kuweka akiba kwa wateja.

 

BENKI ya NMB imerejea na promosheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili ambapo kwa sasa imewatengea washindi zawadi zenye thamani ya Shilingi Milioni 246 zitakazoshindaniwa kwa miezi mitatu.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara NMB, Filbert Mponzi alisema lengo ni kurejesha sehemu ya faida waliyoipata kutoka kwa wateja wao lakini zaidi ni kujenga utamaduni wa Watanzania kuweka akiba benki.

 

Mponzi alifafanua kuwa kampeni hiyi itawawezesha wateja kushinda fedha taslimu na pikipiki za miguu mitatu maarufu kwa jina la Toyo ambapo ni mwendelezo wa kampeni iliyopita ambapo mshindi alijishindia gari jipya aina ya Toyota Fortuner.

 

“Kama mnakumbuka, Awamu ya kwanza ya Bonge la mpango mwaka huu tulipata: Mshindi mmoja wa Toyota Fortuner, watatu wakajinyakulia TATA Mid- sized Pick-up almarufu kama Kirikuu, 24 walioshinda Lifan 3- wheeler (Pikipiki za miguu mitatu) na washindi 120 waliwekewa kiwango cha Sh 100,000 hadi 500,000/- kwenye akaunti zao.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati), akizindua promesheni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, ikiwa na lengo la kuhamashisha nidhamu ya kuweka akiba kwa wateja.

 

“Kikubwa zaidi, katika kampeni hii, zaidi ya shilingi Milioni 246 zitatumika kutoa zawadi kwa washindi, huu ukiwa ni mkakati wetu kama Benki kwa mwaka 2021 ambapo tunakusudia kuendelea kuifanya NMB kuwa chaguo namba moja kwa usalama wa fedha za wateja, suluhisho za kifedha na kwa faida,” alisema Mponzi.

 

Aidha, wateja wote wa NMB wa sasa na wale watakaofungua akaunti mpya wana nafasi ya kushinda zawadi ya Toyo 50 kila moja ikiwa na gharama ya Shilingi Milioni 4.4.  Lakini pia washindi 120 watejishindia kila mmoja Sh 100,000 jumla ikiwa fedha taslimu Shilingi Milioni 12.

 

Wateja wanaofungua akaunti za NMB kwa mara ya kwanza, wakaweka kiasi cha Sh 100,000, au kuhamisha Sh 100,000 kutoka kwenye benki zingine na hata mitandao mingine ya simu watajishindia zawadi mbalimbali kutoka NMB kila wiki na kila mwezi.

 

Kwa wale ambao watafungua akaunti ya NMB au wateja wenye akaunti ya NMB na watakaoweka kiwango cha chini cha Sh 100,000 kwa muda usiopungua mwezi mmoja, watajiongezea nafasi ya kuingia kwenye droo ya finali itakayochezeshwa mwishoni mwa Disemba ambapo Toyo 14 zenye thamani ya Shilingi Milioni 62 zitatolewa.

 

Mponzi alibainisha: “Katika kipindi hiki cha mavuno kwa wateja wetu, tunatoa fursa pia kwa watanzania wote kufungua akaunti kwetu ili kuingia kwenye orodha ya washindi na pia kupata fursa ya  kutunza akiba kwa njia salama zaidi na NMB. Kwa hili, NMB inasema huu ndio Bonge la Mpango awamu ya pili kwa mwaka huu.”

 

Itakumbukwa hivi karibuni Benki ya NMB ilipata tuzo sita za ubora ikionyesha ni benki inayoongoza kwa utoaji huduma bora kwa wateja wake nchini, hivyo ubunifu wa kipekee katika kuhamasisha Watanzania kuwa na utamaduni wa kijiwekea akiba ni miongoni mwa sifa za kipekee za benki hii.

Leave A Reply