The House of Favourite Newspapers

Mambo ni Moto, Infinix Yaja na Kitu Kipya, Uwezo Wake ni Hatari

0
Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa.

 

 

 

Ama kweli hakuna kulala, Kampuni ya simu za mkononi ya Infinix imekuja na kitu kipya kwa wapenzi wa simu zenye ubora aina ya Infinix Zero XPro.

Mtoa huduma wa Infinix (kushoto) akimuelekeza jambo mteja.

 

 

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa amesema siku hiyo ilikuwa ni muhimu kwa Infinix pamoja na wateja wake.

Mteja wa Infinix, Ditrick Kipemba.

 

 

 

Aisha amesema simu hiyo ilizinduliwa tarehe 30 mwezi uliopita ambapo amesema hiyo ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuja na simu hiyo yenye kamera yenye MP 108, 60X Zoom Lens, na pia kuja na amoled screen ya 6.67 4HD.

 

 

 

Aisha amesema lengo na mkutano huo ilikuwa ni kuwashukuru wateja wote walioweza kufanya oda ya awali ya simu hiyo ya kisasa kabisa.

 

 

 

Ameendelea kusema kuwa awali waliagiza kiwango fulani cha mzigo huo lakini kutokana na mapokeo makubwa ya wateja wameamua kuagiza mzigo mkubwa zaidi ili kukidhi haja ya wateja wa simu za kisasa. Afisa huyo alimaliza kuwa kusema kuanzia sasa simu hizo zinapatikana kwenye maduka ya simu nchi nzima.

 

Baada ya Aisha kumaliza kuzungumza Ditric Kipemba mkazi wa Goba, Dar amesema wiki moja iliyopita alikuwa mitaa ya Kariakoo kutafuta simu bora ya kutumia ndipo akakutana na wahudumu wa katika duka la Infinix ambao walimueleza juu ya ujio wa toleo hili jipya.

Baada ya kumueleza ubora wake alifanya oda ya awali (pre oda) na kupatiwa simu hii ambayo ameelezea kufurahishwa kwake na simu hiyo.

Naye Rosemary Massawe mkazi wa Dar amesema baada ya kusikia ujio wa toleo hilo jipya alibadilisha  simu yake aliyokuwa nayo na kuagiza simu hiyo na kueleza furaha yake baada ya kuanza kuitumia na kuona uwezo wake.

Leave A Reply