The House of Favourite Newspapers

Waziri Nape kukutana na Wasanii wa Muziki wa Dansi leo

0

 

1.Mkurugenzi wa Bendi ya The African International 'Twanga pepeta' ASha Baraka (aliyeko mbele) akizungumza na baadhi ya wasani wa muziki wa Dansi.-001

Mkurugenzi wa Bendi ya The African International ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka (wa mbele) akizungumza na baadhi ya wasanii wa Muziki wa Dansi.

2.Wanamuziki wa Dansi wakimsikiliza Asha Baraka alipokuwa akizungumza jambo (pichani hayupo) kabla ya Waziri Nape kufika Ukumbini hapo.-001

Wanamuziki wa Dansi wakimsikiliza Asha Baraka alipokuwa akizungumza jambo (pichani hayupo) kabla ya Waziri Nape kufika ukumbini hapo.

3.Wakongwe wa muziki wa Dansi wakifuatilia kwa makini jambo lililokuwa likizungumzwa na Asha Baraka.-001 Wakongwe wa Muziki wa Dansi wakifuatilia kwa makini jambo lililokuwa likizungumzwa na Asha Baraka.
4.Taswila ya ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya mkutano wa Wasanii wa Muziki wa Dansi na Waziri Nape.-001 Taswira ya ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya mkutano huo.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye, leo jioni anatarajiwa kukutana na wasanii wa Muziki wa Dansi hapa nchini kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya muziki huo.

Mtandao huu umefanikiwa kufika katika Ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo ndipo makutano hayo yatakapokuwepo, na kufanikiwa kukuta maandalizi yakipamba moto, huku wasanii wakongwe wa muziki huo wakijitokeza kwa wingi.

Kabla ya mkutano huo, Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, alikuwa akizungumza na baadhi wa wasanii waliojitokeza katika mkutano huo na kupanga mambo mbalimbali ya kumweleza kiongozi huyo.

(Na Denis Mtima/Gpl)

Leave A Reply