NMB Yakabidhi Hundi Ya Mil 100 Mapambano Dhidi Ya Ugonjwa Wa Corona
Kama mchango wa Benki ya NMB katika kudhibiti na kupambana dhidi ya virusi vya Corona, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna amekabidhi msaada wa kifedha shilingi Milioni 100 kwa Mhe. Waziri Mkuu – Kassim Majaliwa mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Ummy Mwalimu pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali. Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi ya Waziri Mkuu-Dar es Salaam.
Benki ya NMB ikiwa na maadhimio sawa ya kuudhibiti ugonjwa huu, mchango huu utaisaidia serikali katika mapambano dhidi ya virusi hivi. Tunasisitizwa kuendelea kutumia njia stahiki kujikinga na maambukizi.
#Tanzania Bila Corona Inawezekana
#Jikinge Mlinde Mwenzio