The House of Favourite Newspapers

NMB Yatoa Mafunzo Ya Kijasiriamali Kwa Wafanyabiashara Nchini

0

PIC 1

Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo wa NMB – Abdulmajid Nsekela akiongea na wafanyabiashara kwenye hafla ya wajasiliamali ambao ni wateja wa NMB wa wilaya ya Kinondoni. NMB imekuwa ikuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo walio kwenye mtandao wa NMB Business Club kwaajili ya kuongea nao na kupokea maoni yao na mrejesho wa jinsi gani benki inaweza kuboresha huduma kwa wateja zaidi ya wajasiliamali 300 walihudhuria katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni – Mh Paul Makonda.

PIC 2

Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni Mh. Paul Makonda akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa hafla ya Business Club iliyofanyika Sinza jijini Dar es Salaam.

PIC 3

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Vicky Bishubo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni.

Benki ya NMB PLC imetoa mafunzo ya kijasiriamali kwa zaidi ya wafanyabiashara 300 jijini Dar es Salaaam. NMB ina jumla ya vilabu vya biashara 34 nchi nzima vyenye wanachama zaidi ya 10,000. NMB Business Clubs zina malengo ya kuwafikia jamii ya wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa ambao wanajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 50,000 ambao ni wateja wa NMB nchi nzima.

Benki ya NMB PLC imekuwa kipaumbele kuhamasisha wanafanyabiashara nchini kujikimu kimaisha kwa kufungua vituo vya biashara nchini kimoja ambacho kipo kwenye wilaya ya Kinondoni- Sinza Business Centre. Vituo hivi sio sehemu tuu ya kuchukulia mikopo bali pia ni sehemu ya wafanyabiashara kupata ushauri kuhusu mikopo na biashara kutoka kwa wa wataalamu wetu.

Kaimu Afisa wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB PLC alisisitiza kwamba lengo kuu  la vilabu hivi vya biashara vimeundwa  kuhakikisha wafanyabiashara nchini wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.

Akiongea na wafanyabiashara nchini Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni Paul Makonda ameipongeza benki ya NMB kwa kuonyesha shauku ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi kupitia vilabu vya biashara ambavyo vinawapa wananachi elimu ya kijasiriamali na hivyo kupiga hatua ya kuiuchumi kimaisha.

 

 

Leave A Reply