The House of Favourite Newspapers

Nsajigwa Apewa Mikoba ya Matola, Mgunda Taifa Stars

0

NAHODHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Shadrack Nsajigwa ametangazwa rasmi na Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), kuchukua majukumu ya kumsaidia kocha mkuu wa Stars, Kim Poulsen katika nafasi ya kocha msaidizi.

 

Kwa sasa benchi la ufundi la Stars litakuwa kama ifuatavyo; Kocha Mkuu Kim Poulsen, kocha Msaidizi Shadrack Nsajigwa, kocha wa Makipa Ivo Mapunda, Meneja Nadir Haroub Cannavaro, Lisobine Kisongo (Daktari), Gilbert Kigadye (daktari wa viungo), Elieneza Nsanzanzeru (Mwalimu wa viungo), huku John Mashaka na Ally Ruvu wakiwa ni watunza vifaa.

 

Stars sasa inajiandaa na michuano ya kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia la mwaka 2022, itakayofanyika nchini Qatar ambapo Stars ipo kundi moja na timu za Benin, DR Congo na Madagascar.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema: “Ni kweli Kamati ya Ufundi ya TFF imepitisha maboresho yaliyofanyika kwenye benchi la ufundi la Taifa Stars na kuhusiana na kocha Matola na Mgunda ambao walikuwa katika nafasi ya kocha msaidizi, tusubiri kuona ikiwa Kamati itawapangia majukumu mengine.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply