The House of Favourite Newspapers

Zuchu Ampagawisha Kinoma Mama’ke

0

STAA mpya wa Bongo Fleva anayetumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman almaarufu Zuchu amempagawisha kinoma mama yake mzazi, Khadija Kopa au Bi Khadija baada ya kumsikilizisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Yalaa na kuikubali ile mbaya.


Zuchu ameshea video yake na
mama yake wakiwa studio na vaibu kama lote na kuandika;“Familia wamenivamia kwa zombie @s2kizzy (prodyuza). Nimewasikilizisha goma letu jipya, basi ni kama mnavyoona hapo (vaibu la mama yake).

 

Kitendo hicho cha Bi Khadija kupagawa kiasi hicho, basi inaaminika ngoma hiyo itakuwa ni moto wa kuotea mbali.

 

Mashabiki wa Zuchu mara nyingi wameonesha kumuamini anaposema anatoa wimbo mpya kutokana na ubunifu na historia ya nyimbo zake zilizofanya vizuri kama Nyumba Ndogo na Sukari za hivi karibuni ambazo bado ni tishio kutokana na namna zinavyoendelea kuweka rekodi kila kukicha kwenye mitandao ya muziki.

 

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA WIKIENDA umebaini kuwa wimbo huo Zuchu atauachia rasmi Agosti 21, mwaka huu.Juu ya ngoma hiyo mpya, hivi karibuni Zuchu alisema kuwa atakapoiachia, basi anahitaji ulinzi kwani utakuwa ni wimbo wake mkubwa zaidi kuliko zote alizoachia kwa takriban mwaka mmoja na miezi kadhaa aliyodumu kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva.

Leave A Reply