The House of Favourite Newspapers

Nsajigwa Kumrithi Mwambusi Yanga

0

JUMLA ya majina 30 yametuma wasifu (CV) kuomba nafasi ya kuwa kocha msaidizi ndani ya Yanga, huku nahodha na beki wa zamani wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba hiyo.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi aandike barua kuomba kupumzika kwa muda kwa ajili ya kupata matibabu.

 

Uongozi wa timu hiyo, ulitangaza nafasi ya kazi hiyo kwa kuwataka makocha kuwasilisha CV kwa ajili ya kuzipitia kabla ya kumkabidhi kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi, Cedric Kaze kuamua kocha yupi anayemuhitaji.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Yanga ipo katika hatua za mwisho kukamilisha dili hilo la Nsajigwa baada ya viongozi wa timu hiyo kumpendekeza.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa uongozi wa timu hiyo unamuhitaji kocha msaidizi mzawa ambaye anaijua vizuri Ligi Kuu Bara na Nsajigwa ndiye aliyependekezwa kumrithi Mwambusi.Aliongeza kuwa, uongozi unafahamu uwezo wa ufundisha wa kocha huyo ambaye aliwahi kuifundisha timu kubwa na vijana U20 ambayo hivi sasa inafundishwa na Said Maulid.

 

“Uongozi umepokea majina ya makocha 30 ambao wote wametuma CV zao wakiomba nafasi ya kuwa kocha msaidizi na kati ya hao jina la Nsajigwa ndiyo linapewa nafasi kubwa.“

 

Hivyo uongozi upo katika mazungumzo naye ya mwisho na Nsajigwa kama mambo yakienda vizuri, basi atasaini mkataba haraka ndani ya wiki hiii,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mwenyekiti wa mashindano wa Klabu ya Yanga, Thabit Kandoro, juzi alisema: “Mchakato wa kumpata mrithi wa Mwambusi umeanza, hadi sasa nimepokea CV za makocha 30, viongozi inabidi tukutane pamoja na Kocha Kaze kujadili.”Baadhi ya makocha wanaotajwa Yanga ni Shaban Ramadhan, Maalim Seif ‘Romario’, Adolf Rishard na Nizar Khalfan.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

WASHIRIKI wa BSS Watoa BURUDANI ya MWISHO ‘LAIVU’ Kabla ya FAINALI, MADAM RITA Ataja ZAWADI

Leave A Reply