The House of Favourite Newspapers

Nyalandu: Ujasiri Ukaondoe Roho ya Woga, Upendo Uondoe Chuki

0

IKIWA ni siku mbili tangu ajiuzulu uanachama wa CCM na nyadhifa zote ndani ya chama hicho na kuomba kujiunga Chadema, aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amewashukuru Watanzania waliompongeza na kuunga mkono uamuzi wake wa kujiondoa ndani ya chama hicho huku akisema si jambo la busara kuzushiana uongo.

Katika akaunti zake za kijamii za Twitter, Facebook na Instagram Nyalandu ametoa kauli hizo;

“Nawashukuru Watanzania wote walioniletea salamu kuunga mkono uamuzi wangu wa kujiondoa CCM. Turuhusu ushindani na demokrasia ya kweli Tanzania,” amesema Nyalandu.

Ameongeza, “Sijaweza kumjibu kila mtu aliyenitumia salaam, lakini moyo wangu umejaa shukrani kwa wote waliounga mkono uamuzi niliouchukua. Asante! #MunguIbarikiTanzania #letlovelead.”

Aidha Nyalandu ameongeza kuwa hoja zilizo mbele ni kubwa kuliko mtu binafsi na zinalenga kuhusisha utashi wa kila Mtanzania kutafakari na kushiriki kikamilifu safari ya kuijenga na kuiendeleza nchi kidemokrasia, kiuchumi na kijamii.

“Ni maombi yangu kuwa, ujasiri ukaondoe roho ya woga, upendo uondoe chuki, nia njema iondoe kuoneana na kweli ituweke huru na iondoe roho ya kusingiziana kunakoleta kuumizana na sitofahamu ya hali ya juu. Ikawe Heri kwa Watanzania wote. #OneCountry #OneLove #MunguIbarikiTanzania #letlovelead,” amesema Nyalandu.

Nyalandu Ajiuzulu Ubunge, Ajivua Uanachama CCM, Ahamia Chadema

Leave A Reply