BALOZI wa StarTimes Tanzania, ambaye hufanya tafsiri ya filamu za Kichina kwa Lugha ya Kiswahili ambazo hurushwa na StarTimes, Nyamayao ametembelea Ofisi Mpya za Kampuni ya Global Publishers zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Nyamayao ambaye ni mshindi wa mashindano ya Kiswahili ya StarTimes aliambatana na Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Sharobaro ambapo alipata pia fursa nyingine ya kufanyiwa Exclusive interview na Global TV Online. Katika mahojiano hayo, Nyamayao ameanika mengi ikiwemo maisha yake ya sasa na mipango yake ya baadaye.
Picha na Musa Mateja | GPL.