The House of Favourite Newspapers

Polisi Wavamia Mkutano wa Sheikh Ponda, Wakamata Waandishi wa Habari

0

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam limevamia mkutano wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda ambao ulikuwa unatakiwa kufanyika katika hoteli ya Iris, Kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amepanga kuzungumzia sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amethibitisha polisi kuzuia mkutano huo na kusema kuwa baadhi ya waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye ukumbi huo wamekamatwa na polisi.

“Polisi wamevamia mkutano wa Sheikh Issa Ponda katika hoteli ya Iris, Kariakoo. Taarifa za awali zinasema baadhi ya waandishi wamekamatwa. Sheikh Ponda alikuwa azungumze na vyombo vya habari kuhusu suala la Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu asubuhi hii, mara baada ya kurejea kutoka Nairobi ambako alizungumza na Lissu,” alisema Mtatiro.

Aidha Polisi walifika eneo hilo kwa lengo kuzuia mkutano huo usifanyike lakini walikuwa wamechelewa kwani Sheik Ponda alikuwa ameshamaliza kuzungumza na wanahabari, hivyo askari hao waliwakamata baadhi ya wanahabari ambao hata hivyo baadaye waliwaachia.

Sheikh Issa Ponda alikwenda kumtembelea, Tundu Lissu hospitali Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na baadaye kupelekwa Kenya kwa matibabu zaidi.

Baada ya Kuona Hali ya Tundu Lissu, Sheikh Ponda Azungumza Haya

Leave A Reply