The House of Favourite Newspapers

Nyumba na gari, kipi unachotakiwa kumiliki kwanza?

0

IMG-20141025-WA0038
H
uko mtaani kuna misemo mingi ikionesha kuwa, watu wana mitazamo tofauti kuhusiana na suala la umiliki wa mali hizi. Nazungumzia gari na nyumba.

Katika maisha ya sasa, asilimia kubwa ya watu ni vigumu kumiliki gari na nyumba kwa mpigo na ndiyo maana ukijaribu kufuatilia utagundua wapo wanaomiliki magari tena ya kifahari lakini wanaishi kwenye nyumba za kupanga na kuna wenye nyumba lakini hawana usafiri.

nyumbaWakati f’lani niliwasikia vijana wakibishana juu ya hili. Kwamba kati ya gari na nyumba, kipi ambacho mtu anastahili kumiliki. Yupo aliyesema kuwa, kwenye ulimwengu huu kuna baba mwenye nyumba lakini hakuna baba mwenye gari. Huyo alimaanisha kuwa, kuanza kuwa na nyumba unapata heshima zaidi.

Mwingine akasema, eti ukiwa na nyumba yako hata iwe ya kifahari vipi, kisha ukawa unakatiza mtaani ukipigwa na jua huku ukitoka jasho na vumbi la barabarani likikupiga, huwezi kuheshimika.

Tofauti na yule ambaye mtaani anatanua na gari la kifahari kisha jioni akirudi anaingia kwenye nyumba ya kupanga.

Lakini wapo waliokwenda mbele zaidi kwa kuhoji kwamba, inakuwaje mtu amiliki gari la kifahari kisha awe amepanga kwenye chumba tena kimoja? Hayo ni maswali yanayoibuka inapokuja hoja ya kipi cha kumiliki kwanza kati ya hivyo viwili.

Hata hivyo, leo nataka angalau niwape elimu kidogo kuhusiana na hili. Ukweli ni kwamba usafiri na nyumba vyote vina umuhimu wake lakini kila mmoja ana nafasi ya kuchagua kile ambacho anaona kinafaa kukimiliki kwanza.

Mimi kama mimi naweza kukushauri kwamba, kama unaishi kwenye nyumba nzuri yenye ‘parking’, ambayo hulipi kodi kubwa na iko karibu kabisa na eneo unalofanyia kazi zako, sioni tatizo kama utaanza kumiliki gari.

Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, hakikisha unaishi maisha mazuri leo kabla ya kujiandalia kesho yako ambayo huna uhakika nayo.

Sasa ukiwa unaishi kwenye nyumba ambayo inakufanya ujisikie vizuri licha ya kwamba unalipia, kisha ukawa na usafiri wako, mazingira hayo yanaweza kukufanya ukaanza kuitengeneza kesho yako vizuri.

Namaanisha kwamba, baada ya kuona mambo yako yanakwenda vizuri, hata ukitaka sasa kwenda kununua kiwanja mbali, hutakuwa na tatizo la usafiri, utakuwa unatumia gari lako kwenda kutafuta kiwanja na hata ukiwa umeanza ujenzi, ni rahisi kuwa unakwenda mara kwa mara kufuatilia ujenzi na usafiri wako pia unaweza kukusaidia kusafirishia vifaa vya ujenzi.

Lakini kwa upande mwengine sasa, kama unaona nyumba ya kupanga unayoishi ina matatizo na unalipa kodi kubwa, yaani hujisikii poa kabisa, kutakuwa na haja gani kuanza kufikiria suala la kununua gari?

Katika mazingira hayo ndipo utapata hasira za kuwa na nyumba yako na hapo ndipo unaweza kusema, nyumba kwanza, usafiri baadaye.

Kwa kuhitimisha niseme tu kwamba, uamuzi wa nini uanze kumiliki unatokana na mazingira unayoishi hivyo ni uamuzi wako uanze na kipi na kama unaweza kumiliki vyote  ni heri.

Leave A Reply