The House of Favourite Newspapers

Obama Amponda Trump “Mbinu Anazotumia Kukabiliana na #Covid19 Hazisaidii”

0

Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama amemtuhumu Rais Donald Trump kuwa ameshindwa kuikabili #COVID19 kwani mbinu anazotumia hazijasaidia chochote hivyo ni miongoni mwa wanaopaswa kulaumiwa kwa vifo vingi vilivyotokea.

 

Mpaka tarehe 9 Mei 2020, Marekani kumetokea vifo vya watu zaidi ya 77,000 vilivyotokana na #Corona huku Maambukizi yakifikia zaidi ya milioni 1.2.

 

Obama amesema, takwimu hizo zimeweka rekodi ya juu kabisa katika uso wa dunia kutokana na Trump kushindwa kujua namna ya kuwaokoa Wamarekani kutokana na janga hilo.

 

Trump aliahidi kuwa, mpaka mwezi Februari mwaka huu, ugonjwa huo ungekuwa umemalizwa kabisa ndani ya mipaka ya Taifa hilo lakini ilipofika katikati ya Machi, Trump alieleza kwamba ugonjwa huo umekuwa ukisambaa kwa kiwango cha juu ndani ya nchi.

 

Ikulu ya Marekani imemtetea Trump kwamba amekuwa akifanya kazi kubwa kuhakikisha anakabiliana na corona na kwamba, ameliokoa Taifa hilo kutumbukia katika janga kubwa zaidi.

Leave A Reply