Ofisa TAKUKURU Amuua ‘Girlfriend’ Wake kwa Risasi -Video

OFISA Msaidizi (mlinzi) wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, James Paulo (27),  anadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi tatu kichwani, mchumba wake ambaye alikuwa akitarajia kumuoa.

 

Taarifa za awali zinadai kuwa, James alikuwa akimsomesha mtarajiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Beatha Kafuru, ngazi ya diploma, kozi ya ‘nursing’ na kwamba licha ya kujaliwa kupata mtoto mmoja, inadaiwa baada ya masomo, mtarajiwa wake alikataa kufunga ndoa, ndipo kijana huyo alipochukua maamuzi ya kumuua.

Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi. Mauaji hayo yametokea katika nyumba wanayoishi.

 

Polisi imeeleza kuwa imeikuta bunduki aina ya Browning ambayo ni mali ya Takukuru ikiwa na risasi nne na maganda matatu.


Loading...

Toa comment