The House of Favourite Newspapers

OFM yatumbua jipu la Tanesco Moro

0

Dustan Shekidele, Moro
Watanyooka! Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers imeungana na Rais John Pombe Magufuli katika kutumbua majipu ya uovu kwenye jamii ambapo imewaingiza matatani mainjinia wa Shirika la Umeme (Tanesco) mjini hapa baada ya kudaiwa kuunganisha umeme kwenye kibanda cha wakala wa mitandao ya simu kinyume na utaratibu hivyo kuhatarisha maisha ya watu.

Awali, OFM ilipokea malalamiko kutoka kwa madereva, makondakta, abiria na wafanyabiashara kutoka kwenye stendi ndogo ya daladala mjini hapa hivi karibuni kuwa katika eneo lao kuna jipu la kutumbuliwa kwani kuna hatari ya watu kupoteza maisha kufuatia kitendo cha Tanesco kuunganisha umeme kwenye kibanda ambacho unaweza kukiinua na kuondoka nacho.

Baada ya kupokea malalamiko hayo kisha kufika eneo la tukio, OFM ilipiga picha za mnato na kufanya mahojiano na mashuhuda wa ishu hiyo huku binti aliyekutwa ndani ya kibanda hicho akiendelea kutoa huduma.

“Ninavyojua hiki kibanda kinamilikiwa na jamaa anayeitwa Daud, sasa kuhusu mambo ya kuunganishiwa umeme labda Tanesco watuambie kulikoni,” alisema mmoja wa wafanyabiashara wadogo wa eneo hilo.

Baada ya kuona hatari hiyo, mwanahabari wetu alibisha hodi kwenye ofisi ya Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro ambapo kwa mujibu wa skretari wake aliyejitambulisha kwa jina moja la Lucy, meneja huyo alikuwa safarini hivyo aliyekuwepo ni Kaimu Meneja, Injinia Luti Misana ambaye alipoelezwa juu ya tukio hilo alionesha kushtushwa mno.

Kaimu meneja huyo alimwagiza fundi wao aongozane na OFM hadi eneo la tukio, walipofika na kujionea uungwanishwaji huo wa umeme alimpelekea ripoti mkuu wake aliyeahidi kumfikisha mhusika kwenye vyombo vya sheria.

Leave A Reply